Miti inayo tuzunguka, ina nguvu nyingi sana za kiroho. Ukiwa na ufahamu juu ya nguvu za kiroho zinazopatikana ndani ya miti mbalimbali, basi maisha yako ya hapa duniani yatakuwa rahisi sana. Leo nitaelezea miti michache pamoja na nguvu za kiroho iliyo nazo. Unga wa alovera. Huwekwa kwenye chupa maalumu na kufukiwa ama kuzikwa kaburini kwa ajili ya kuwanyamazisha watu wanao zungumza uongo na uovu kuhusu wewe. Unga wa muagrimonia : Unga huu ni moja kati ya dawa zenye nguvu kubwa sana za kiroho, kazi yake kubwa ni kurudisha laana na uchawi kwa mtu aliye utuma kwako. Unga wa mualfafa.
Huwekwa nyumbani kujilinda dhidi ya umasikini na kufilisika, pia huwekwa kwenye chombo maalumu na kisha kwenda nao benki au kwa mtu yoyote Yule kwa ajili ya kupata mkopo wa fedha. Unga wa Mvuaza : Hutumika kwa ajili ya kumpumbaza mtu au kuwapumbaza watu. Husaidia pia kujilinda dhidi ya majambazi na kushinda kesi Unga wa mfausiku : Una matumizi mengi sana si rahisi kuyataja yote hapa. Unga wa mti wa mlufakale. Hutumika kurefusha umri wa kuishi. Hutumiwa sana na wachawi na ndio sababu wachawi wengi huishi miaka mingi sana. Hutumika katika biashara, mapenzi, mahusiano, kazi, uongozi na kadhalika, kwa ajili ya kudumisha jambo lililokusudiwa, yaani kama ni ndoa basi iwe ya kudumu na kama ni mapenzi yawe yadumu na yasife na kama ni biashara iwe ya kudumu na isife. Unga wa mualikani: Kazi kubwa ya dawa hii ni kukomesha uchawi uliotumwa kwako kwa ajili ya kukutia umasikini, kukufilisi au kukusababishia matatizo ya kifedha.
Ngekewa : Ngekewa sio mti, ni manyoya ya mnyama apatikanae porini, mnyama huyu hufanana na Ndezi, au Panya Buku. Manyoya ya mnyama huyu hutumika kuvuta wateja katika biashara na kuongeza bahati katika mambo mbalimbali kama vile sanaa na kadhalika, Unga wa Viungo vya aina zote kama vile karafuu, pilipili manga n.k. matunda mbegu na matunda jamii ya karanga : Hutumika katika tambiko maalumu la kuleta mafanikio katika biashara, pamoja na kuongeza bahati katika biashara . Unga wa mualtea Hutumika kuwaita malaika wazuri katika nyumba, pamoja na kuongeza uwezo wa mtu wa kiroho ama wa kuona mambo yaliyo rohoni. Kwa mfano kama kuna siri Fulani kuhusu mtu Fulani (mathalani mke au mume wako ) unataka kuijua, unachotakiwa ni kutumia unga huu huku ukifanya manuizo maalumu, usiku wa siku hiyo utaonyeshwa siri unazo taka kuzijua kupitia ndoto.
Pia hukupa uwezo wa kun'gamua mahali vilipo vitu vilivyo potea, utakupa uwezo wa kujua mambo yanayo tokea sehemu nyingine. Kwa mfano, wewe unaishi Dar Es salaam, na familia yako inaishi Mbeya, unaweza kujua mambo yanayo endelea huko kupitia nguvu ya unga huu. . Muangelica : Unga wa mti huu husaidia kuwalinda wanawake pamoja na watoto dhidi ya uovu wowote. Wanawake wajawazito wanashauriwa kutumia unga unga huu ili kujilinda dhidi ya jicho ovu. . Muanisi : Ni unga unaotumika kumkinga mtu dhidi ya jicho ovu na uchawi.
Sunday, 4 March 2018
JIFUNZE MITI YENYE UWEZO MKUBWA 01
Tags
Artikel Terkait
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

EmoticonEmoticon